Baada ya Rais kuzindua programu ya vijana ya jenga kesho iliyobora (BBT) iliyochini ya wizara ya kilimo yenye lengo la kutoa ajira kwa vijana zaidi ya milioni tatu,Spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametaka vijana kujengwa kifra ili kuamini kilimo ni sehemu ya ajira.
Dkt. Tulia ametoa ushauri huo jijini Dodoma kwenye Programu maalum ya mikopo ya kilimo kwa wanawake na vijana inayotolewa na TADB bila riba ambapo amesema vijana wengi wamekuwa wakiamini kilimo ni sehemu ya waliokosa kazi za kufanya “Ni muhimu kuendelea kuzungumza na vijana mtu asione kwamba naenda kwenye kilimo kwakuwa nimekosa sehemu zingine zote”