Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea tarehe 22/2/2023 Jijini Dar es Salaam, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya afya yake kuimarika.
Meneja uhusiano MOI, Patrick Mvungi amesema..”Milanzi alipokelewa MOI tarehe 22/2/2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A”
“Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia ambapo ataendelea na huduma kama Mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili”
“Tunatoa shukran za dhati kwa Watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza Osam Milanzi”