Licha ya marufuku ya maandamanao nchini Senegal, muungano wa Upinzani nchini humo, Yawwi Askan Wi, umesiistiza kushiriki maandamano hii leo Jumatano na kesho Alhamis wakati wa kesi ya kiongozi wake Ousmane Sonko.
Juma lililopita wafuasi wa Sonko na polisi walikabiliana kwa kile amcaho sonko anadai pilisi walikuwa na njama ya kumuangamiza.
Tayari watu 4 wanakisiwa kuwa wanachama wa kundi la Casamance wamekamatwa wengine 19 wakisakwa kile polisi wamesema wamejihusha na kutatiza usalama wa taifa.
Kutokana na taharuki inayoshuhudiwa nchini humo vyuo vikuu na shule zimefungwa.
Nchi kadhaa barani Afrika zimekuwa zikifanya maandamano katika siku za karibuni kulalamikia kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha haswa bei ya vyakula ikionekana kupanda.
Sonko, mkaguzi wa kodi mwenye umri wa miaka 46 ambaye alishika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 15 ya kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2019, anapata uungaji mkono mkubwa miongoni mwa vijana wa Senegal.
Anakabiliwa na uchunguzi baada ya kuvuliwa kinga yake ya ubunge.