Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, amesema Ofisi yake imebaini Wakusanyaji mapato katika Mamlaka 98 za Serikali za Mitaa hawakuwasilisha jumla ya Bilioni 11.07 katika akaunti husika za Benki kutokana na ufatiliaji duni na kutofanyika kwa usuluhisho wa hesabu mara kwa mara.
Kichere pia amesema licha ya Wakusanyaji mapato katika Mamlaka 98 kutowasilisha Bilioni 11.07, Mawakala wa Mapato katika Mamlaka nyingine 10 za Serikali za Mitaa pia hawakuwasilisha Benki kiasi cha Shilingi Bilioni 4.12.
Kufuatia mapato hayo kutowasilishwa, CAG amewashauri Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha fedha zote ambazo hazikuwasilishwa zinawasilishwa na kuwekwa Benki.