Chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Manyara, kimewafikia wakinamama wajawazito katika hospitali ya Tumaini pamoja na watoto wenye uhitaji jumuishi iliyopo wilaya ya Hanang ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kwa kuwapatia misaada huku ukiwa ni utaratibu wa Chama hicho kuifikia jamii.
Judith Benson Kiongozi wa chama cha Afya Tughe Mkoa wa Manyara amesema chama hicho kimeamua kumfikia mtu ambae hakuweza kufikiwa —“Tumeamua kuwajibika kama kinamama kupitia chama cha Afya na serikali Tughe Mkoa wa Manyara kuzifikia jamii hizi”
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi baada ya kupokea misaada hiyo Matilda Shio Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kateshi A amesema–“Tunawashukuru Tughe kwa kutambua wapo watu wa namna hii na kuwatia Moyo, shule hii inawanafunzi jumuishi wapo wenye mahitaji maalumu hivyo zawadi walizotoa leo ni baraka kwao,lakini pia tunaishukuru Serikali kwa namna ya pekee inavyoiangalia shule hii kwa pekee kwa kupatia walimu pamoja na miundombinu, wito wangu jamii isiwafiche watoto wenye uhitaji maalumu “
Nae Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Hanang Dokta Peter Patrick amesema jambo hilo linawatia matumaini wagonjwa kuona wanafikiwa na jamii na amkpongeza juhudi za chama hicho huku akisema misaada hiyo itakwenda kupunguza changamoto ziilizopo ikiwemo Mashuka kwa wagongwa hivyo itakwenda kuboresha.