Kampuni ya Asas nchini imesema kuwa licha ya takwimu kuonyesh unywaji wa maziwa nchini Tanzania bado upo chini kulinganisha na nchi nyingine bado wanaendelea kuwashauri watanzania kunywa maziwa kwa afya.
Akizungumza na Millardayo.com & Ayo TV Mkurugenzi wa Asas, Ahmed Asas alisema “Kuna umuhimu sana wa unywaji wa maziwa kwa watu kwani kitaalamu kwa mujibu wa Shirika la afya duniani ( WHO) wanasema binadamu anapaswa anywe maziwa walau lita 200 kwa mwaka”
“Kiutaalamu wanashauri maziwa bora ni yale yaliyosindikwa na usindikaji sio kutumia kemikali,maziwa yetu yanachemshwa kuwekwa katika vifungashio vizuri na kuongezewa radha,”amesema
“Maziwa yetu ni mazuri sana kwa afya na virutubisho vinavyopatikana vinaongeza virutubisho ambavyo mwili vinahitaji tunashauri kila mtanzania anywe maziwa walau hata lita moja kwa siku,”amesema