Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Jenista Joakim Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) leo Ikulu Dar es salaam, akichukua nafasi George Boniface Simbachawene.
Rais Samia pia amemuapisha George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akichukua nafasi ya Jenista J. Mhagama.