Wakati Serikali ikiendelea kuhamasisha uwekezaji na viwanda Taasisi inayohusika na maboresho katika mamlaka za serikali za mitaa ambayo ni Umoja wa Makatibu tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa nchini (TOA) inatarajia kuwa na mkutano wa 13 wa mwaka wenye lengo la kuhamasisha kukuza sekta ya uwekezaji na viwanda nchini.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma Mwenyekiti wa umoja huo Albert Msovela amesema Mkutano huo unatarajiwa kuanza April 04 hadi 06,2023 jijini Dodoma unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt.Samia Suluhu Hassan.
“Dhima ya mkutano huu mkuu wa 13 ni kuhamasisha uwekezaji na viwanda kupitia mamlaka za serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ambapo wadau mbalimbali kutoa serikali na sekta binafasi wanatarajia kushiriki na mada mbalimbali zitawasilishwa”alisema Msovela
Msovela amesema TOA imejipanga kuhamasisha usimamizi na uboreshaji wa utoaji huduma za jamii kama vile afya, elimu, kilimo, biashara, miundombinu na maji, usimamizi wa rasilimali watu, fedha, miradi ya maendeleo pamoja na utawala bora na kuweka kipaumbele katika kuibua miradi ili kuongeza tija badala ya serikali kuu kufanya kila kitu.
“Tunaona kuwa ipo haja kwa sasa miradai yote ambayo inaanzishwa na serikali wananchi ndiyo wawe waibujai wakuu ili miradai hiyo iwe endelevu tofauti na ilivyo sasa miradi mingi inakosa tija kutokana na kushindwa kushirikisha wananchi”–alisema
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TOA kwa pamoja wamekubaliana kumpatia tuzo Rais Samia kutokana na juhudi zake za utendaji wa kazi kwa kutafuta pesa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake.