Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete amewataka Wakulima Kuzingatia maelekezo ya watabiri wa Hali ya hewa ili kulima kilimo chenye tija kuondokana na changamoto ya kupanda mazao ambayo hayaendani na Hali ya hewa na kupelekea kupata hasara.
NAIBU Waziri Mwakibete amesema Wakulima wengi wamekua wakipuuzia utabiri wa Hali hewa unatolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ( TMA) na kupata Changamoto katika sekta hiyo .
Hayo ameyabainisha katika kikao cha baraza wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA) kilichofanyika Mkoani Morogoro kikiwa na lengo la kujadili bajeti na utekelezaji wake
Katika hatua nyingine amewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) kuongeza juhudi na kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa mapato ili kupunguza utegemezi kutoka serikalini
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA) Dk.Burhani Nyenzi alibainisha changamoto ya maslahi duni kwa watumishi hali inayopelekea wataalamu wengi kuhama taasisi nyengine.
Aidha licha ya Mamlaka hiyo kua na Changamoto lakini wameendelea kupata hati Safi ya matumizi ya fedha kutokana na ripoti ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)
Kwa Upande wao Baadhi ya Wakulima mkoani Morogoro wamepongeza kazi nayofanywa na TMA na kwamba utabiri wao umekua msaada kwao kutokana na mabadiliko tabia nchi ambayo yamepelekea Hali ya hewa kubadilika
Baraza hilo la Wafanyakazi wa TMA limeahidi kufanya kazi bora zaidi na kuomba kuwezeshwa kwa Wafanyakazi kutekeleza Majukumu yao kwa Ufanisi kulingana na taaluma zao kwa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mishahara kupendekezwa.