Mahakama katika mji wa kaskazini wa Kano nchini Nigeria imeamuru kuchinjwa kwa jogoo siku ya Ijumaa baada ya malalamiko ya majirani kuhusu kuharibu mazingira kwa kelele
Mahakama hiyo ilitangaza jogoo kuwa kero katika mtaa huo baada ya kuwika mara kwa mara ambapo majirani wawili walisema walikosa usingizi kwa sababu ya jogoo huyo
Mmiliki wa jogoo huyo ambaye awali alipewa sharti la kuhakikisha amamfungia ndani jogoo huyo akashindwa sasa ameamriwa kuhakikisha anamchinja kuku huyo siku ya Ijumaa vinginevyo atakabiliwa na adhabu