Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewataka wasaidizi wa Rais kutotumia lina la Rais kwa dhikaha wakati wakijibu hoja za wabunge wakati wa vikao vya bunge kwasababu kiongozi wa nchi amekasimu madaraka kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara 35 (1).
Maelekezo ya Spika ameyatoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka Kaomba mwongozo wa Spika chini ya kanuni ya 76 kanuni ndogo ya tisa kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha dkt. Mwigulu Nchemba wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu Esther Matiko kuhusu pesa zinazoidhinishwa kutekeleza shughuli za serikali kushindwa kwenda kutumika ipasavyo ,akijibu hoja hiyo Waziri wa fedha na Mipango dkt. Mwigulu Nchemba amesema “Hakuna malipo ya kila mwezi yanayoweza kufanyika bila Rais kujua”
Spika Dkt. Tulia amesema “Kwa mwongozo wa katiba na kanuni zetu malipo yale yanafanywa na maafisa waliopewa kazi hiyo ya kulipa na sio Rais kwahiyo lile neno idhini,Rais ndiye anayeidhinisha malipo katiba yetu imeshaweka wazi”