Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Kilumbe Ng’enda amesema Serikali inakwamisha maendeleo ya watu kwa kuchelewa kutoa vitambulisho vya Taifa kutokana na baadhi ya watanzania kukwama kwa kukosa vitambulisho hivyo
Ng’enda amesema hayo wakati akichangia hoja ya waziri mkuu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.
“Leo ni mwaka wa 10 nataka serikali ielewe wapo watu wanataka kuingiza umeme majumbani kwao wanaombwa kadi za NIDA,wapo watu wanataka kuingiza maji,wapo watu wanataka kuingia kwenye mfumo ea TRA,wapo wanaomba Passport za kusafiria lakini wanakwamwa kwaajili ya vitambulisho vya Taifa”–Mbunge wa Kigoma Mjini Kilumbe Ng’enda