Shekhe Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir amewataka waislamu nchini pamoja na taasisi za dini hiyo kuwatumia wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kuzifikia fursa za kimaendeleo zilizopo Ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi.
Rai hiyo ameitoa wakati wa kongamano la maendeleo ya waislamu nchini lililofanyika mkoani Tanga amesema kuwa ili waweze kuimarika kiuchumi ni lazima wahakikishe wanawatumia wataalamu waliopo Nchini.
Amesema kuwa kwa miaka mingi Taasisi za dini ya kiislamu pamoja na waumini wake wameshindwa kuwatumia wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya kiuchumi.
“Sasa wakati umefika Kwa Waislamu ikiwemo na taasisi zake kuwatumia wataalamu waliopo hapa nchini Kwa ajili ya kuweza kujiletea maendeleo ikiwemo kukamatia fursa za kiuchumi zilizopo”amesema Mufti Zubeir.
Hata hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Surumbu amesema kuwa Serikali Mkoani hapo ipo tayari kutoa Ushirikiano kwa Taasisi zote za dini katika Shughuli za kimaendeleo.
Nae Mratibu wa Ujenzi wa Mradi wa Hospitali Ayub Kidege amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kutoka na michango mbalimbali ya waislamu.