Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe leo April 10 kimechambua ripoti ya CAG ambapo pamoja na mambo mengine kimeitaka DART kuingia mkataba mara moja na TPDC kubadilisha Mabasi ya Mwendokasi kutoka kutumia
Diseli na kutumia gesi asilia (CNG).
Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo, Zitto Kabwe amenukuliwa akisema “Katika Ripoti ya Mwaka 2021/2022, CAG ametoa hoja mbili kubwa za ukaguzi kuhusu Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya Mabasi ya Mwendokasi Dares Salaam (DART); ujenzi kutokidhi ubora wa viwango na matumizi ya dizeli badala ya gesi kwenye mabasi ya mradi huo”
“Kuhusu eneo la dizeli, CAG amebaini kuwa TPDC imeingia gharama ya ujenzi wa miundombinu kujaza gesi asilia kwenve mabasi va mwendokasi bila ya kuwa na mkataba na
DART, Kwa mujibu wa CAG, DART waligoma kuingia mkataba na TPDC kwa ajili ya kubadilisha magari kutoka mfumo wa mafuta kwenda gesi kwa madai kuwa wameingia mkataba wa miaka 12 na kampuni ya kuuza mafuta ya dizeli”
“Hoja hi ya mkataba wa miaka 12 haina mashiko na ni kichaka cha ubadhirifu, taarifa tulizonazo zinaonesha kwamba DART wanatumia wastani wa lita 30,000 za diseli kuendesha huduma ya usafiri kwa siku, hui ni sawa na kutumia Shilingi milioni 91 kila siku, sawa na shilingi bilioni 33 kwa mwaka mzima”