Mchakato huo unajiri takriban miezi saba baada ya maandamano ya nchi nzima yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini kilichotokea mwezi Septemba akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Mwanamke huyo wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22 alikamatwa kwa madai ya kukaidi sheria kali ya mavazi kwa wanawake.
Yakianzishwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, majadaliano bungeni yalipelekea kupitishwa siku ya Jumapili kwa kanuni za jumla za mswada uliotajwa kuwa “wa kuzuia madhara kwa wanawake na kuboresha usalama wao dhidi ya tabia mbaya, IRNA
Mswada huo ambao unaweza kufanyiwa marekebisho, unaweza kusainiwa rasmi na kuwa sheria katika miezi ijayo.