Mitchell Bock, 30, alisema alianza mbinu ya kuacha kutegemea dawa za kupunguza mfadhaiko ( depression )polepole, na hivi majuzi aliacha kutumia dawa yake ya kupunguza wasiwasi kutokana na mbinu ya kuoga kwenye maji yenye baridi kali Aliiambia Daily
Kabla ya kuanza njia hiyo ya jumla, alipata wasiwasi mkubwa na msongo wa mawazo kwa miaka kumi na alilazwa hospitalini baada ya jaribio la kujiua.
Alianza kutafiti mbinu mbadala na mama yake ili kuona ikiwa kulikuwa na njia tofauti za kuboresha afya yake ya akili.
Wiki kadhaa baada ya kulazwa hospitalini, mama yake alimnunulia beseni la kuogea lenye barafu, na Bock akaitumia mara moja kwa kuoga ndani yake.
Ingawa ilikuwa ngumu kwake mwanzoni, alianza kuzoea utaratibu wa baridi.
“Nilipofanya hivyo mara ya kwanza, nakumbuka niliamka bila hisia za kawaida za kuogopa. Ilikuwa ni kama kwenda kulala na mafua na kuamka nikiwa mzima kabisa,’ alieleza.
Kama sehemu ya shughuli zake za kila siku, Bock hujaribu kuoga kwenye barafu kila siku, na wakati mwingine ataogelea kwenye baridi kali na matokeo hayo ya kila siku yamemsaidia kutumia kiwango kidogo cha dawa na hata kuacha kuhudhuria vipindi vya matibabu.