Chanjo hiyo inayoitwa R21 – inaonekana kuwa na ufanisi mkubwa, tofauti kabisa na jaribio la awali katika eneo hilo ambayo imeelezwa na wanasayansi walioitengeneza kuwa ni mabadiliko ya ulimwengu.
Wadhibiti wa dawa nchini Ghana wametathimini data ya majaribio ya mwisho kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo, ambayo bado haijaonekana hadharani, na wameamua kuitumia.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa, kwa wastani bara la Afrika linarekodi kesi milioni 200 na vifo 400,000 kwa mwaka vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria.
Ugonjwa wa malaria huua takribani watu 620,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa ni watoto wadogo.
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Ghana, ambayo imeona takwimu hizo, imeidhinisha matumizi ya chanjo hiyo kwa watoto wenye umri wa kati ya miezi mitano hadi miaka mitatu.
Taasisi ya Serum ya India inajiandaa kuzalisha kati ya dozi milioni 100-200 kwa mwaka, na kiwanda cha chanjo kinajengwa Accra, Ghana.
Malaria husababishwa na vimelea na huambukizwa kwa binadamu kupitia mbu jike aina ya Anopheles ingawa ugonjwa huu unaweza kuzuilika na kutibika, au kusababisha kifo usipotibiwa.