Serikali mkoani Tanga imewaomba viongozi wa dini kuendelea kushirikia nao katika kukemea ndoa za jinsia Moja hapa nchini Ili kulinda Mila na tamaduni za kitanzania.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakati wa iftar iliyoandaliwa na shirika la bima la Taifa .
Amesema kuwa viongozi wa dini wanajukumu la kuendelea kielimisha waumini wao juu ya athari za matendo yasiyo mpendeza mungu katika jamii.
“Mkoa wetu na nchi Kwa ujumla Sasa tupo kwenye janga la ndoa za jinsia Moja sambamba na kishamiri Kwa vitendo vya ushoga tunaomba viongozi wa dini tushirikiane katika vita hii Ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kubaki salama”amesema DC Mgandilwa.
Nae Shekhe wa mkoa wa Tanga Jumaa Luuuchu amesema kuwa wao viongozi wa dini wanakemea vikali vitendo hivyo na kuwataka wazazi na walezi kurudi katika kulea watoto katika maadili yaliyo mazuri.
“Matokeo ya matendo haya maovu ni.kutokana na ukimya uliofanywa na wazazi wakati watoto wao walivyokuwa wameanza kuvaa nguo Kwa mitindo isiyofaa lakini Sasa wakati umefika tuimarishe malezi ya watoto wetu katika nyanja zote”amesema Shk Luuuchu.
Aidha Mwakilishi wa Mkurungenzi Mkuu wa bima nchini Herman Mushi amesema kuwa kwa Sasa shirika hilo limepunguza madai ya malipo ya fidia na Sasa yanalipwa ndani ya siku Saba toka majanga kutokea.