Takwimu za FAO kuhusu uzalishaji wa asali nchini Iran zinakuja huku takwimu za wizara ya kilimo ya Iran zilizotolewa mwezi Aprili mwaka jana zikionyesha kuwa uzalishaji wa kila mwaka wa asali nchini umefikia tani 111,000 na takwimu hizo zilionyesha kuwa Iran ilikuwa ya tano kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya nyuki duniani mwaka jana ikiwa na makoloni takriban milioni 11 katika mashamba karibu 100,000.
Takwimu za Chama cha Wafanyabiashara cha Iran zinaonyesha Iran iliuza asali ya thamani ya dola milioni 5.6 kwa nchi 22 duniani mwaka jana.
Mauzo ya asali kutoka Iran yanatarajiwa kuongezeka angalau mara mbili mwaka huu huku kukiwa na mipango ya kusambaza bidhaa hiyo nchini China chini ya mkataba uliotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwaka jana.
Kwa mujibu wa Press TV, FAO imeitaja asali inayozalishwa nchini Iran kuwa bora zaidi duniani, ubora ambayo imesema unatokana na maliasili ya nchi hiyo na aina zake za mimea huku mamlaka zilisema mwezi Februari kuwa mauzo ya asali nchini China yatawapa wafugaji nyuki wa Iran fursa ya kuuza bidhaa zao katika nchi nyingine za Asia Mashariki.
Takwimu za FAO zilizoangaziwa katika ripoti ya Jumatatu zilionyesha kuwa wafugaji wa nyuki wa Iran wamezalisha takriban tani 77,000 za asali mwaka jana na uzalishaji huu wa asali uliiweka Iran nyuma ya China na Uturuki katika orodha ya kimataifa ya wazalishaji wakubwa wa asali mwaka 2022.