Polisi wa Italy wamepata tani mbili ya dawa za kulevya aina ya cocaine zikielea kwenye bahari karibu na ufukwe wa mashariki mwa kisiwa cha Italy cha Cicily na wachunguzi wanakisia kwamba mzigo huo uliachwa baharini na meli ya kubebea mizigo, kwa mpango wa kutumia boti nyingine ndogo kuuleta kwenye nchi kavu ngawa maafisa hawakusema ni kundi gani, kama lipo, lililoshukiwa..
Polisi wanaoshughulika na masuala ya fedha wa Italy walikadiria kwamba kasha hilo ambalo lilikuwa limefungwa kwa plastiki lina thamani ya euro milioni 400 ambazo ni karibu dola milioni 450 za kimarekani, kwa bei ya mtaani.
Polisi walitumia ndege karibu na mahala kasha hilo lilipopatikana, ili kuchunguza iwapo kulikuwa na mengine yalioachwa baharini pia imesemekana kuwa uhalifu uliopangwa katika kisiwa cha Sicily kwa muda mrefu umetawaliwa na kikundi cha Cosa Nostra kikundi cha mafia chenye nguvu zaidi nchini Italia, Cosa Nostra kina mikuki inayofika Marekani na kote ulimwenguni.
Mnamo Januari, viongozi wa Italia walimkamata mmoja wa waanzilishi wakuu wa kikundi hicho, Matteo Messina Denaro, baada ya msako wa miaka 30.
Leo, biashara ya dawa za kulevya nchini Italia, na sehemu kubwa ya Ulaya, inaongozwa na kikundi cha uhalifu cha ‘Ndrangheta, chenye makao yake katika milima ya Calabria, kwenye bara la Italia karibu na Sicily.
Kwa ujumla polisi walihesabu zaidi ya paketi 1,600 za cocaine zikiwa zimefungwa kwe vivurushi 70, taarifa imeongeza.