Polisi wa India waliwataja wanandoa hao kuwa ni Hemubhai Makwana mwenye umri wa miaka 38 na mkewe Hansaben Makwana, 35, na walisema miili yao isiyo na vichwa iligunduliwa na watoto wao wenye umri wa miaka 12 na 13. Sadaka hiyo ya ibada ilitokea nyumbani kwao katika kijiji cha Vinchiya. iliyoko katika wilaya ya Rajkot ya jimbo la magharibi la Gujarat, kama ilivyoripotiwa na jarda Ła MEAWW.
Wanandoa hao walipatikana wakiwa wamekufa na watoto wao baada ya kushiriki katika walichokiita ibada ya dhabihu ya kitamaduni iliyowahitaji kujikata kichwa kwa kutumia guillotine[ mashine ya kujinyongea hasa kukata kichwa ]ya kujitengenezea nyumbani.
Inspekta mdogo wa Polisi wa Vinchhiya, Indrajeetsinh Jadeja alisema wanandoa hao walikuwa wakifanya “ibada” ya dhabihu ambayo iliwahitaji kuwasha madhabahu ya moto kabla ya kuweka vichwa vyao kwenye guillotine ya kujitengenezea nyumbani iliyoshikiliwa na kamba.
Akasema, “Mara tu walipoifungua ile kamba, upanga wa chuma ukawaangukia, ukawakata vichwa vyao, na kuvitupa motoni lakini Watoto wao walimtembelea mjomba wao katika kijiji cha jirani wakati kitendo hicho kiovu kilipotokea’’.
Mamlaka ilisema wanandoa hao walikuwa wamewatuma watoto wao katika kijiji cha karibu siku moja kabla na walipata maandishi ya kujitoa mhanga kwa Kigujarati, ambayo yalisema wanandoa hao walikuwa wamejiua kwa hiari. Hakuna mtu mwingine aliyehusika katika vifo vyao.
Inasemekana kwamba barua hiyo iliwasihi jamaa zao kuwatunza wazazi wazee wa wenzi hao na watoto wawili.
Jina “guillotine” lilianzia miaka ya 1790 na Mapinduzi ya Ufaransa, lakini mashine kama hizo za unyongaji zilikuwa tayari zimekuwepo kwa karne nyingi.