NI April 19, 2023 ambapo Watangazaji wawili Maulid Kitenge na Gerald Hando wameingia kwenye vichwa vya habari baada ya wawili hao kujiunga na kituo cha Radio cha Wasafi.
Wawili hao watakuwa wakisikika kupitia Kipindi cha Asubuhi kinachorushwa katika Radio hiyo kiitwacho Habari za Asubuhi ‘Good Morning’.
Hapo awali wawili hao walikuwa wakisikika kupitia kituo cha Majizzo kiitwacho EFM.
Sasa kutokana na kile kilichotokea leo mashabiki ama wadau wamehoji kuhusu kile alichowahi kukiandika Majizzo March 25, 2023, stori kamili unaweza ukabonyeza play kurahamu zaidi.