Mashindano ya watoto ya kuwinda paka nchini New Zealand yamehirishwa kufuatia mvutano kuhusu tukio hilo.
Waandaaji wa shindano hilo wa kila mwaka walikosolewa baada ya kutangaza kitengo kipya cha watoto kuwinda paka mwitu na kuwaua nchini New Zealand.
Vijana waliambiwa wasiue wanyama wa kufugwa, lakini walihimizwa vinginevyo waue paka wengi wa mwituni ili wapate zawadi ya $155, sawa na Tsh 356000 Tukio hilo lilileta shutuma kutoka kwa vikundi vya ustawi wa wanyama.
Siku ya Jumanne, Jumuiya ya Kuzuia Ukatili kwa Wanyama ya New Zealand ilisema kuwa imefarijiwa “mpango wa watoto ambao ulihusisha kuwapiga risasi paka mwitu” hautaendelea.