Mwanaharakati wa Mazingira Shamim Nyanda kushirikiana na Ubalozi wa Netherland wameshiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya Sekondari ya Makumbusho ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mfalme William Alexander Akizungumza na Waandishi wa Habari mwanaharakati huyo amewaasa Wananchi kuhakikisha kuwa wanatunza mazingira na kuhifadhi kwa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Ni Jukumu letu sote kuhifadhi Mazingira ni jukumu letu sote kupanda miti na sio kupanda miti tu pia kuitunza, sisi kama shirika tumechukua jukumu la kurudi hapa shuleni baada ya miezi mitatu kwaajiri ya kuwatunza wale wanafunzi ambao watakuwa wameweza kuhifadhi miti yao vizuri” Shamimu Nyanda
Kaimu Balozi wa Uholanzi Tanzania, Job Runhaar akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji miti ameiasa Jamii kutunza na kuhifadhi mazingira ambapo mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi ni ya kila mmoja katika Jamii.