Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Hassan ametoa msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto Hisani Orphanage Centre, kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumza katika shughuli hiyo, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni ambaye amemuwakilisha Mh. Naibu Waziri, amewaasa watoto hao kutokata tamaa na kumuomba Mungu awape ujasiri, kusoma na kufanya kazi kwa bidii na pia kufuata utaribu.
Aidha amesema kuwa Wizara inajitahidi kuhakikisha kwamba watoto wanalindwa na pia kuhakikisha Ustawi wao.
“Wizara inajitahidi sana kuhakikisha kwamba tunalinda watoto, tunahakikisha ustawi wao” amesema Dkt. Nyoni.
Baada ya kuzungumza na watoto, Dkt. Nyoni pamoja na msaidizi wa Mh. Naibu Waziri Baraka Lucas, wamekabidhi mahitaji Muhimu kwa watoto katika kituo hicho.