Kutokana na changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo uchomaji wa moto na kilimo katika bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Fatma amesema sasa rasmi bwawa hilo litalindwa na jeshi la wananchi kushirikiana Jeshi la akiba.
Mwassa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti rafiki ya maji inayotekelezwa na Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu ambapo amesema Serikali haitavumilia mtu atakayebainika kujihususisha kwa namna yeyote na vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa kuchoma moto au kufanya shughuli nyingine za kibinadamu atachukuliwa hatua ikiwemo kifungo cha miaka saba Gerezani.
Amesema katika kuhakikisha eneo hilo linalindwa na tayari Jeshi la Wananchi kushirikiana na jeshi la akiba wamepewa kazi hiyo ya ulinzi na kuwepo eneo hilo usiku na mchana kwani awalo eneo hilo lilipandwa miti zaidi ya laki mbili lakini badae Watu wasiojulikana wakachoma moto.
Katika hatua nyingine RC Mwassa amewataka Wananchi kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi na kujenga kwani Sheria za Uhifadhi wa vyanzo vya mji zipo na Zinafanya kazi atakayebainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake kwa mujibu wa sheria ya mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu Elibarik Mmassy amesema bwawa hilo linategemewa na wakazi Wa Morogoro kwa zaidi ya asilimia sabini kwa huduma ya maji.
Mmasy anasema kampeni hiyo inalenga kupanda miti milioni 2 katika maeneo mbalimba ya vyanzo vya maji mkoa wa Morogoro ambapo kwa siku ya uzinduzi miti elfu mbili imepandwa .
Amsema kwasasa bwawa la hilo linakabiliwa na changamoto ya shughuli za kibinadamu na kusababisha tope kujaa katika bwawa na kuleta changamoto ya upungufu wa maji mji wa Morogoro
Naye balozi namba moja wa Mazingira Msanii Afande Sele amesema serikali inapaswa kusimamia utekelezaji na usimamizi wa sheria ili kukomesha tabia hiyo.
Afande Sele anasema kinachoonekana ni uzembe wa baadhi wa wasimamizi wa sheria kwani Wananchi wamekuwa wakipuuza sheria zilizowekwa na Serikali.