Ray Houghton, mwenye umri wa miaka 65 kutoka jiji la Manchester nchini Uingereza, amewashangaza watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba Alitumia zaidi ya $ 10,000 sawa na Tsh Mil 23,460,000 kuchorwa tattoo mwili mzima.
Alianza kujichora tattoo katika mwili wake akiwa na umri mdogo, enzi hizo akifanya kazi jeshini na sasa akiwa na umri wa miaka 65 mwili wake wote umefunikwa na tattoos hata sehemu zake za siri ambazo zilimgharimupesa nying katika maisha yake yote.
Houghton aliiambia South West News Service kwamba alitaka kuchora sehemu zake za siri “kwa muda, mrefu lakini mtaalamu wa uchoraji alikataa kufanya hivyo.
Lakini mara tu alipompata bwana mwingine wa kuchora tattoo, Houghton alichora maeneo yake ya yote.
Mjenga misuli huyo alikiri kwamba anapata jumbe nyingi kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa watu wanaotaka kuona sehemu zake za siri zilizochorwa tattoo.