Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamomwaka 1964 na kuanzishwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika,hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.
Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 kisha tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaamna kubadilishana Hati za Muungano.
Waasisi walibadilishana Kanuni za Misingi za Muungano na kuchanganya udongo wa Tanganyika na ule wa kutoka Zanzibar kuwa ni ishara ya muungano wa nchi mbili hayati Mwalimu Julius Kambarage alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mheshimiwa Sheikh Abeid Amani Karume aliekuwa Makamu wa kwanza wa Rais, na Mzee Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho ya Mwaka huu yanaadhimishwa katika ngazi ya Mikoa na Wilaya kwa kushiriki shughuli za kijamii na uzinduzi wa miradi ya maendeleo na kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu”
Rais Dkt. Samia ameelekeza shughuli za maadhimisho hayo zifanyike kuanzia tarehe 17 Aprili, 2023 hadi siku ya kilele tarehe 26 Aprili, 2023.
Mheshimiwa Majaliwa pia amesema kuwa maadhimisho hayo ambayo yatafanyika kupitia Mikoa, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama yaambatane na uzinduzi wa miradi ya maendeleo, shughuli za kijamii hususan upandaji miti, usafi wa mazingira na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali. Muungano 59!
Kwa muungano wa huu kwenye Bara la Afrika imewezekana kuungana kwa mataifa mawili huru yanayojitawala n tukio hili limeonyesha kwamba kuwa na dhamira ya dhati na kuwa na ari na moyo kwa watu wa Afrika na viongozi wao, inawezekana kuwa na umoja wa Afrika.
Tanganyika na Zanzibar ndiyo umoja pekee ambao bado unaendelea miongoni mwa miungano adimu sana duniani kote.