Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema kuwa Tanga Kwa Sasa sio mahali salama Kwa bidhaa za magendo sambamba na madawa ya kulevya .
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa boti maalum ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa za magendo Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa hapa.
Amesema kuwa mkoa huo kama ni komborera tayari mpira umeshabutuliwa hivyo tutakuwa wakali sana katika kudhibiti magendo Ili kutoruhusu mapato kupotea”amesema RC Kindamba.
Hata hivyo ameitaka TRA mkoani hapa kutumia njia rafiki katika ukusanyaji wa Mapato ikiwemo kufanya maridhiano Ili wafanyabiashara waweze kulipa kwa Kodi kwa hiari yao.
Hata hivyo Naibu Kamishna wa forodha na ushauri Geofrey Katundu amesema kuwa katika kipindi Cha kuanzia Julai hadi Disemba mwaka jana bidhaa za magendo zenye thamani ya sh Bil 11.05 ziliweza kukamatwa ambapo baada ya tozo na adhabu ziliweza kulipiwa sh Bl 13.1.
“Kwa mkoa wa Tanga pekee bidhaa za magendo zenye thamani ya sh Mil 675 ziliweza kukamatwa ambapo baada ya tozo na adhabu ziliweza kulipiwa sh Mil 799.”amesema Katundu.
Aidha amesema kuwa ununuzi wa boti hiyo yenye thamani ya sh Mil 529 itakwenda kuwa mkombozi katika jitihada za kudhibiti vitendo vya ukwepaji wa Kodi kupitia bidhaa za magendo.