Ili kupambana na soko la ajira nchini na kuhamasisha vijana kujiajiri, Serikali imesema itaanzisha programu mbalimbali za kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia kilimo cha Mkonge na sekta nzima kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema hayo jijini Tanga leo alipotembelea katika Ofisi za Bodi ya Mkonge (TSB) ambapo pamoja na mambo mengine alikagua majengo ya ofisi hizo na kuzungumza na watumishi.
“Zao la mkonge ni zao la kimkakati kwa ajili ya BBT (Building Better Tomorrow), kama mnavyofahamu Mheshimiwa Rais alianzisha programu hiyo ya Jenga Kesho Iliyo Bora kwa ajili ya vijana na Mkonge upo kwa ajili ya kuzalisha ajira kwa vijana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania, Saddy Kambona amesema Bodi ina mikakati mingi ya kuhakikisha inafikia malengo ya serikali ya kuongeza uzalishaji kutoka tani 36,000 mwaka 2020 hadi 120,000 ifikapo 2025.
Amesema zao la Mkonge ni moja ya mazao yenye fursa nyingi za ajira zitakazoweza kubadili maisha yao na kuachana na zile pilika pilika za kutembea na bahasha kutafuta ajira baada ya kutoka chuoni.
“Kwa hiyo tutaandaa programu maalumu kutoka wataalamu wenye utaalamu wa kutosha kufundisha ni namna gani tunaweza kutumia mabaki ya mkonge kwenye kujitengenezea fursa mbalimbali kama kilimo cha uyoga kwa mfano, ufugaji wa mende na miradi mingine midogo midogo ambayo haihitaji mitaji mikubwa kwa vijana wetu kuweza kujikomboa.
“Hivyo tunatarajia kuanza na Klabu za Mkonge kwenye mashule ambapo tutaanza na Shule ya Sekondari ya Coastal kwa majaribio na baadaye tutakwenda kwa vijana wengi zaidi kuona kwamba wanaweza kulima mkonge na kutumia mabaki ya mkonge wakalima uyoga kupitia mabaki hayo Mkonge na uyoga una soko zuri