Wadau wa uvuvi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kusitisha mpango wa kufunga ziwa Tanganyika kwa kutaja hatua hiyo kuathiri hali ya kiuchumi kutokana na idadi kubwa ya watu kutumia ziwa hilo kama njia pekee ya kujipatia kipato.
Wakizungumza na Ayo TV wameeleza kabla ya ziwa Tanganyika kufungwa kwa muda wa miezi mitatu Serikali na wadau wanapaswa kutungeneza njia mbadala itakayowawezesha wananchi kuendelea kupata kipato kwa kipindi hicho.
Licha ya mchakato huo kushirikisha wadau wa Uvuvi lakini yapo matakwa kadhaa ambayo yalipendekezwa kama sehemu mbadala ya kiuchumi ambayo yanatajwa hadi sasa ikiwa zimebaki takribani siku 17 hayajafanyika.
Kufuatia hatua hiyo chama cha NCCR mageuzi kimeeleza kwenda Mahakamani kufungua kesi kupinga zoezi la kufunga ziwa Tanganyika kwa madai ya mkataba huo kukinzana na sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003.
“Ikiwa Waziri Ulenga hatotoa tamko la kusitisha utekelezaji wa huo mkataba ndani ya wiki moja sisi tunaenda mahakamani kuzuia huo mkataba kama NCCR na tunaanza mikutano maeneo yote ya ziwa Tanganyika kuwafahamisha kwamba wizara ya Uvuvi inataka kuisariti sheria yake yenyewe,tutaenda kujenga ufahamu wa kutosha kwa wananchi”–>Frank Ruhasha – katibu mwenezi wa NCCR Taifa
Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka ya ziwa Tanganyika LTA inaeleza zoezi hilo kufayika kwa lengo la kutunza mazalia ya Samaki ambayo yameharibiwa kutokana na Uvuvi haramu.