Meneja wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa wa Arusha Mhandisi Laynas Sanya ametoa ripoti ya mtandao wa barabara wenye kilometa zaidi ya 5000 katika Wilaya sita zilizopo katika mkoa huo.
Katika taarifa hiyo Mhandisi Laynas amesema kati ya kilometa 5000 za mtandao wa barabara hizo barabara zinazopitika hadi sasa ni asilimia 17 ambazo zinazopitika kwa hali ya kuridhisha ni asilimia 30 na zaidi ya asilimia 52 zinazopitika kwa shida.
Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasana ilipoingia madarakani iliongeza bajeti kutoka shilingi bilioni 8.2 hadi kufikia bajeti ya shilingi bilioni 19.6 bajeti ambayo lipelekea kuongeza mtandao wa barabara za lami, changalawe na kupunguza barabara za udongo.
pia ameeleza changamoto wanazo kutananazo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayopelekea kuwepo kwa mvua nyingi zinazo haribu miundo mbinu ya barabara na wameanza kuchukua hatua kwa kufanya mabadiliko madogo kwenyemikataba ya mwaka huu wa fedha, na kwamaeneo ambayo yameathirika zaidi wamewasiliana na uongozi wa TARURA makao makuu Ili kuweza Kupata fedha za ziada.