Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, takriban wakimbizi 20,000 wamehifadhiwa katika kambi moja iliyoko kijiji cha Koufron nchini Chad huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto inaripotiwa kuwa mbaya.
Kambi hii iko mita mia chache kutoka Darfur Magharibi, moja ya majimbo ya Sudan ambapo wengi wamekimbilia nchi jirani ya Chad na kulazimika kuwa wakimbizi ili kunusuru maisha yao.
Tangu Aprili 15, mapigano yanaendelea nchini Sudan kati ya vikosi vya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdul Fattah al-Barhan na wanamgambo wa vikosi vya radiamali ya haraka (RSF) vinavyoongozwa na Jenerali Mohammad Hamdan Daghlo.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu mia moja wameuawa huko Darfur Magharibi tangu wiki moja iliyopita.
Kutokana na kukosekana mazingira mwafaka ya upashaji habari kuna uwezekano idadi ya vifo ikawa ni kubwa zaidi na wakimbizi hao wanalazimika kutumia mitandio ya kichwa ya wanawake kujihifadhi na joto.
Aidha wanatumia vigogo vya miti na nyasi ili kutengeneza sehemu za kupatia hifadhi.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeripoti kuwa hali ya wakimbizi hao kutoka Sudan walioko nchini Chad ni mbaya kwani pia imeelezwa kuwa baadhi ya wakimbizi walioko nchini Chad wameweza kuhama makwao na baadhi ya vitu vyao.