Afisa wa polisi wa zamani wa Minneapolis Tou Thao amepatikana na hatia ya shtaka la kusababisha mauaji ya bila kukusudia, yaliyotokana na kifo cha 2020 cha George Floyd.
Jaji wa ene la Hennepin Peter Cahill alitoa uamuzi wa hatia Jumatatu usiku, akiandika katika uamuzi wake, “Uamuzi huo unatokana na kupatikana kwa ukweli na hitimisho la sheria.”
Uamuzi huo unakuja takriban miaka mitatu baada ya kifo cha Floyd mnamo Mei 25, 2020, mikononi mwa maafisa wa polisi na kusababisha maandamano nchini kote.
Thao ndiye wa mwisho kati ya maafisa wanne wa polisi waliofutwa kazi Minneapolis kupatikana na hatia katika kesi hiyo.
“Hukumu ya Tou Thao ni ya kihistoria na ni matokeo sahihi,” Mwanasheria Mkuu wa Minnesota Keith Ellison alisema katika taarifa yake.
“Inaleta kipimo kimoja zaidi cha uwajibikaji katika kifo cha kutisha cha George Floyd. Uwajibikaji si haki, lakini ni hatua ya kuelekea kwenye haki.”
Tarehe ya hukumu ya Thao rasmi kuwa Agosti 7 na huukumu ya Thao inatarajiwa kuwa kati ya miezi 41 na 57 jela.
Thao mwenye umri wa miaka 37 tayari ametiwa hatiani kwa mashtaka ya shirikisho ya kukiuka haki za kiraia za Floyd na kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 3 na nusu jela.
Thao ni mmoja wa maafisa wanne wa zamani waliokabiliwa na mashtaka ya serikali na shirikisho katika kifo cha Floyd, akiwemo Derek Chauvin mwenye umri wa miaka 47, ambaye alinaswa kwenye video ya usalama na kushuhudia picha za simu ikionesha goti polisi huyo juu ya shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika 9, na kumfanya kupoteza fahamu na bila mapigo ya moyo na Floyd baadaye alitangazwa kuwa amefariki hospitalini.