Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amefanya ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar ikiwemo eneo la tawi la CCM Mbweni, ukumbi wa CCM Maisara Social Hall , nyumba ya CCM kumbukumbu ya Afro Shiraz eneo la Posta Kijangwani pia alikutana na familia ya Hayati Nahoda ambao wanaoishi eneo hilo na mwisho kituo cha mafuta Kinazini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Huu ni mwendelezo wa ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ngazi zote.
Dk.Mwinyi amesema baada ya muda mfupi miradi yote ya uwekezaji itaanza kwa fursa zilizopo kwenye miradi hiyo kwa uendelezaji pamoja na maboresho ya ofisi za CCM.