Rais Felix Tshisekedi Jumatatu alitangaza siku ya maombolezo ya kitaifa na timu ya mawaziri inatazamiwa kusafiri hadi eneo hilo kuratibu misaada ya kibinadamu na usimamizi wa majanga, msemaji wa serikali Patrick Muyaya alisema.
Msimu wa sasa wa mvua, kawaida kwa eneo la Kivu Kusini, unatarajiwa kudumu hadi mwisho wa Mei.
Watu wengi wameripotiwa kupotea baada ya mvua kusababisha mito kufurika tarehe 4 Mei, katika mkoa wa Kalehe huku shughuli za uokoaji zikiendelea
Kufikia sasa miili 400 imeopolewa kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyokumba vijiji viwili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki iliyopita.
Mamlaka hapo awali ilisema watu 200 walikufa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku ya Alhamisi
Katika vijiji kadhaa vilivyo karibu na ufuo wa Ziwa Kivu, watu wamekuwa wakichimba tope kwa mikono katika harakati za kuwatafuta jamaa waliopotea.
Wafanyakazi wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu wa Congo hawana mifuko ya kuhifadhi miili.
Wanalazimika kuirundika miili iliyofunikwa kwa blanketi katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi katika jimbo la Kivu Kusini.
Maafa hayo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalikuja siku mbili baada ya mafuriko kuua takriban watu 131 na kuharibu maelfu ya nyumba katika nchi jirani ya Rwanda, ambayo iko ng’ambo ya Ziwa Kivu.
Ni siku tatu sasa tangu mafuriko yalipotokea na idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka, sasa imefikia 394.
Mama mmoja aliyefadhaika huko Nyamukubi alisema mumewe alikuwa amenusurika na alikuwa amelazwa hospitalini lakini watoto wake wote hawajulikani walipo.
“Ni kama mwisho wa dunia,” Gentille Ndagijimana mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia alipoteza wazazi wake na dada zake wawili, aliliambia shirika la habari la AFP.
Katika kijiji cha Bushushu baadhi ya majengo ambayo bado yamesimama nusu yamezikwa kwenye tope.
Wiki iliyopita nchi jirani ya Rwanda pia ilikumbwa na mafuriko baada ya Ziwa Kivu kuvunja kingo zake na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 130.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mafuriko hayo ni kielelezo kingine cha kuongeza kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa.