Jopo la majaji watano nchini Nigeria siku ya Jumatatu walikaa kikao cha kwanza kusikiliza kesi inayowahusisha viongozi wa upinzani walioshiriki uchaguzi wa mkuu wa rais wa mwezi Februari ambao chama tawala kilishinda.
Tangu Nigeria irejee kwenye demokrasia mwaka 1999 miongo mitatu baada ya utawala wa kijeshi, uchaguzi umekuwa ukiishia mahakamani, ingawa hakuna pingamizi iliyowahi kutengua matokeo.
Malalamiko ya kupinga ushindi wa Bola Tinubu yaliwasilishwa mwezi Machi pamoja na wagombea kadhaa wa urais akiwemo kiongozi mkuu wa upinzani Atiku Abubakar aliyeshika nafasi ya pili na mtu wa nje Peter Obi aliyeshika nafasi ya tatu.
Mahakama ina siku 180 za kutoa hukumu tangu maombi yalipowasilishwa, na pia ina uwezo wa kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi.
Hakuna uamuzi mkubwa uliotarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu.
Abubakar, ambaye alikuwa katika azma yake ya sita ya kuwania urais, alidai katika ombi lake kwamba alishinda uchaguzi huo uliofanyika tarehe 25 Februari.
Wote Abubakar na Obi walidai kuwa matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwa ni batili kutokana kwa “kutofuata” sheria za uchaguzi na “vitendo vya rushwa”.
Abubakar, anayejulikana nchini Nigeria kama “Atiku”, pia alidai katika ombi lake la kurasa 223 kwamba Tinubu alishindwa kupata kizingiti cha kisheria cha asilimia 25 ya kura kutoka makao makuu wa nchi hiyo.
Katika ombi lake, Obi, ambaye aliungwaji mkono kwa kiasi kikubwa na vijana wa Nigeria, pia alidai kushinda uchaguzi huo.
Hata hivyo mapambano yanayoendelea mahakamani hayawezi kuzuia kuapishwa kwa Tinubu tarehe29 mwezi Mei. Tinubu ni mrithi wa aliyekuwa raisi wa Nigeria Muhammadu Buhari aliyekuwa madarakani kwa mihula miwili.