Hivi majuzi daktari mmoja wa Brazil alishangaza mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii kwa kuchapisha picha ya eksirei ya mwanamume anayeugua ugonjwa wa cysticercosis[saistisercosis] ambaye mwili wake ulikuwa umejaa mayai ya minyoo.
Mwezi uliopita, Daktari Vitor Borin katika Hospitali ya das Clínicas huko , Sao Paulo, alichapisha picha ya X-ray ya mgonjwa kwenye Twitter ili kuwaonyesha wafuasi wake jinsi maambukizi ya minyoo yanaweza kuwa mabaya.
Daktari alieleza kuwa madoa hayo meupe yanayoonekana katikati ya sehemu yake na mikononi mwake yalikuwa mayai ya minyoo baada ya kuambukizwa na vimelea vya kawaida vya utumbo.
Kwa bahati nzuri, mgonjwa, ambaye alikuja kwenye uchunguzi kufuatia kikohozi cha muda mrefu hakuwa na hatari yoyote kutokana na mayai hayo kwani alipewa huduma ya haraka na hayakuwa tishio kwa afya ya mwanamume huyo, bali yalizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii ya Brazili.
Mayai ya minyoo ya tegu huenezwa kupitia chakula, maji, au sehemu zilizochafuliwa na kinyesi. Wanadamu humeza mayai wakati wanakula chakula kilichochafuliwa au kutia vidole vilivyoambukizwa kinywani mwao.