Polisi katika kaunti ya Kwale wanachunguza kanisa moja eneo la Vumbu baada ya tetesi kuibuka kuwa linaendeleza itikadi za kidini zisizoeleweka.
Kanisa la Rainbow Faith Ministries lililopo eneo la msitu linadaiwa kuwa makazi ya mamia ya waumini na familia ya kiongozi wake Mzee Mdata Nyamawi.
Kanisa hilo lilifunguliwa mwaka wa 2017 na linashutumiwa kwa kuwahujumu waumini.
Baadhi ya waumini hao wanadaiwa kuacha kazi zao zenye malipo mazuri katika makampuni makubwa na kwenda kukaa huko kuabudu na kufanya kazi za mikono.
Waumini wote wa kanisa hili wanaamini maneno ya wanachosema ni Nabii wao Joyce Mkumbi mwenye umri wa miaka 23, wa nyakati za mwisho zinazohitaji watu kukusanyika na kuabudu pamoja kila siku.
Wengine wameacha nyumba zao na kuanza maisha yai kanisani humo, wakisema wanaepuka mizozo ya familia.
“Tunaamini kwamba ni ujumbe wa kweli kutoka kwa Mungu, hivyo ujumbe wowote anaotutumia kupitia kwake tutatii kwa sababu ndiyo maana tuko hapa,” Simon Mboga, mwanachama mwingine, alisema.
Naibu kamishna akizungumzia tukio hilo alisema;
“Hali hii inaweza kwanza kuwa hatari kwa afya kwa sababu tuna choo kimoja au viwili tu na mkurupuko wa kipindupindu ni rahisi sana kutokea,” Lotiatia Kipkech, Naibu Kamishna wa Kaunti ya Msambweni, alisema.
Siku ya jana Viongozi sita wa kanisa la Rainbow Faith Ministries, lililopo ndani kabisa ya msitu wa Vumbu katika eneo la Msambweni, kaunti ya Kwale, walifikishwa mahakamani.
“Hali hii inaweza kwanza kuwa hatari kwa afya kwa sababu tuna choo kimoja au viwili tu na mkurupuko wa kipindupindu ni rahisi sana kutokea,” Lotiatia Kipkech,
Mnamo Jumapili Jioni, maafisa wa DCI walivamia majengo ya kanisa hilo na kuwakamata sita hao, ambao ni wanachama wa kamati ya usimamizi ya kanisa hilo. Wengine watatu walikamatwa lakini hawakufikishwa mahakamani
Mkurugenzi wa DCI wa Kwale Wasike alisema kuwa sita hao watafunguliwa mashtaka ya uasi na kuwanyima watoto faragha, miongoni mwa mashtaka mengine.
Kiongozi wa kanisa hilo mwenye umri wa miaka 26, ‘Prophetess’ Joyce Mukumbi, Jumatatu alipelekwa katika hospitali ya Port Reitz mjini Mombasa kwa uchunguzi wa kiakili. Lakini Madaktari wa magonjwa ya akili walikataa kufanya hivyo, wakisema wanahitaji kwanza amri ya mahakama.
Ngumbao na Nguma walisema wananyanyaswa kwa sababu ya imani yao walisema hawajafanya kosa lolote na kwamba tuhuma dhidi yao kuwanyima watoto chakula, elimu na huduma za afya ni za uongo.
“Watoto wetu huenda shuleni na hospitali wanapougua. Tunajua kuna maadui waliotumwa na bwana wao shetani ili kuhakikisha neno la Mungu halihubiriwi,” Ngumbao alisema.