Kampuni ya Google imeanzaa kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe ambapo kwa miaka minne walikua wakifanyia kazi ili kufanikisha mpango wa kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe.
Magari hayo yatakuwa na vitufe vya kusimama na kujiendesha ila zaidi ya hapo hakuna kingine chochote mfano usukani na breki, vyote hivyo hauvioni kama ilivyo kawaida kwenye magari ya kawaida.
Ukiwa ndani ya hili gari unaweza kusoma gazeti au kufanya kingine chochote kama vile kufanya kazi kwenye laptop ambapo muonekano wake pia umetengenezwa kiubunifu kiasi kwamba utasaidia watu wasiyaogope kwa kuanzia kwenye muonekano pia wayakubali kirahisi, yani yana muonekano wa kirafiki.
Mgunduzi msaidizi wa magari hayo Sergey Brin amebainisha mipango hiyo jijini California Marekani na kwamba magari haya yataanza kufanya kazi na kumilikiwa na watu wanaoyahitaji ndani ya mwaka mmoja ujao.
Pamoja na hatua hii watafiti wanachunguza juu ya uwezekano wa kutumika kwa teknolojia hii mpya ambapo tayari magari haya yametengenezwa na kufikia idadi ya mamia lakini hayazidi elfu moja.
Ungependa stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.
Swali ni je…. utakua huru kuendeshwa na hili gari mitaa kama Kariakoo?
Tazama video yake hapa chini.