Ni Mei 10, 2023 ambapo Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally alipata wasaa wa kutembelea Makao Makuu ya Benki ya CRDB na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Abdulmajid Nsekela.
Mufti pia aliweza kushiriki uzinduzi wa mikopo maalum ya Hija na Umrah, unaotolewa #CRDBAlBarakahBanking ambao unalenga kuwawezesha waislamu kufikia malengo yao ya ibada hiyo kwa gharama nafuu.
Mufti, aliipongeza CRDB BAnk kwa kuanzisha mikopo hiyo ya ufadhili wa Hija na Umrah, huku akiwahamasisha Waislam kote nchini kutumia fursa hiyo kutimiza ibada za Hija na Umrah.