Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe amefariki dunia leo asubuhi Katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya ameithibitishia @ayotv_ kuhusu kifo cha Membe ambapo amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa Hospitali Alfajiri ya leo na baadaye akafariki.