Mzee mwenye umri wa miaka 72 nchini China aliteka mioyo ya mamilioni ya watu baada ya kuripotiwa kuwa hutumia muda wake mwingi kutangaza vipodozi na bidhaa nyingine za urembo mtandaoni ili kumtibu mjukuu wake mgonjwa.
Kupitia chapisho kwenye jarida la oddity Zhu Yunchang mwenye umri wa miaka 72 ni mfano kamili ya aina ya watu wanaofanya kila aina zaidi kwa wapendwa wao, Mstaafu huyo wa China amekuwa akitumia muda wake mwingi katika kazi yake ya urembo wa kujipodoa kwenye mitandao ambayo hutumia kila aina ya bidhaa za urembo, kuanzia creams , lipstick na mascara na bidhaa nyingine za urembo kwaajili ya kuonyesha mashabiki kote nchini.
Miaka sita iliyopita, mjukuu wa Zhu Yunchang, Xiao Jingyan, aligundulika kuwa na ugonjwa adimu na wa kudhoofika kwa misuli ya mgongo (SMAs),mvulana huyo alikuwa na umri wa miaka mitano tu wakati huo, na madaktari walikadiria kuwa alikuwa na miezi 18 tu ya kuishi.
Lakini Zhu alizidi kuwa na matarajio ya kumsaidia na amekuwa akipambana na hali yake tangu wakati huo, kwa msaada wa familia yake lakini haikuwa vita rahisi.
Dawa pekee inayotumika kutibu hali ya Xiao inaweza tu kuagizwa kutoka Marekani na kugharimu karibu yuan 700,000 ($100,000) sawa na tsh 235,800,000 mill.
familia ya Xiao Jingyan waliamua kufanya lolote kuokoa maisha yake, hivyo wakauza nyumba yao na kukopa pesa nyingi kadri walivyoweza, lakini bado hazikutosha hapo ndipo babu wa kijana huyo alipoamua kujihusisha na masuala ya make up mtandaoni na kuingia kwenye blog ya urembo.
Mara tu baada ya kuanza kurusha clip zake moja kwa moja, umaarufu wa mtandaoni wa Zhu Yunchang ulianza, na akaanza kumtafutia mjukuu wake malipo mazuri lakini wakati fulani, ufuasi wake haukuongezeka , na watu wakaanza kumshutumu binti yake kwa kuchukua nafasi yake ili kupata huruma ya watu na kupata pesa. Bado, Zhu aliendelea kupost video zake .
“Ikiwa mjukuu wangu anaweza kutembea kama mtoto wa kawaida, nitahisi utulivu nitakapofumba macho yangu,” babu mwenye kujali na bora alisema.