Mkuu wa Sera za Nje za Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametangaza kuwa gharama za kijeshi za umoja huo zimeongezeka kwa asilimia 30.
Borrell ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la mawaziri wa nchi za umoja huo na za maeneo ya Bahari ya Hindi na Pasifiki lililofanyika katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm na akabainisha kuwa gharama za kijeshi za Umoja wa Ulaya zimeongezeka kwa asilimia 30 tangu mwaka 2014.
Hayo yanaripotiwa huku Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) ikitangaza kuwa chimbuko la ongezeko la gharama za fedha katika uga wa kijeshi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya katika mwaka 2022 limetokana na vita vya Ukraine na wataalamu wengi pamoja na waangalizi wa kimataifa wanaamini kuwa ung’ang’anizi wa Magharibi hasa Marekani wa kupanua wigo wa satua za shirika la kijeshi la NATO ndio uliosababisha hali hiyo.