Mwanamtandao maarufu Nchini Tanzania William Malecela maarufu kama ‘LeMutuz’ ambaye pia ni Mmiliki wa Online TV ya LeMutuz amefariki dunia leo Jijini Dar es salaam.
Taarifa za kifo cha LeMutuz ambaye ni Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania John Malecela zimethibitishwa na Ofisi yake pamoja na baadhi ya Ndugu zake.
Mmoja wa Ndugu hao ameiambia @AyoTV_ kuwa wanasubiri taarifa rasmi ya familia ili Vyombo vya habari vipewe taarifa kamili juu ya kifo hicho cha Rafiki wa wengi Ndugu LeMutuz.
Na Miongoni mwa waliotoa Pole kwa Familia ya Malecela ni Kampuni ya Asas ambayo Marehemu alikuwa ni miongoni mwa mabalozi waliopata fursa kuitangaza vyema bidhaa ya Asas.
Asas wameandika..‘Tunasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Balozi wetu Bw.William Malecela (Le-Mutuz) kilichotokea leo Mei 14, 2023 jijini Dar es Salaam, tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wetu’- Kampuni ya Asas