Mkazi wa Burns Beach aliandika barua hiyo akiomba jirani yao, Kylie, afunge dirisha lao wakati wa kupika nyama.
Barua hiyo iliwasilishwa kwa Hey Perth kwenye Facebook. Barua hiyo inasomeka: “Habari jirani, tafadhali unaweza kufunga dirisha la upande wako unapopika?” Familia yangu ni watumiaji wa mboga mboga,[vegan] tunakula vyakula vya mimea tu na harufu ya nyama unayopika hutufanya tuhisi kichefuchefu na kufadhaika tutashukuru kuelewa kwako – asante. Sarah, Wayne, na watoto.”
Hata hivyo, barua hiyo ilizua kizaazaa na gumzo kwa mamia ya watoa maoni wakisema kuwa walishangazwa na barua hiyo na kuhisi kama jirani huyo alikuwa akijibu kwa hasira kupita kiasi.
comment baada ya barua hiyo zilisomeka hivi;
“Mungu! 🤣🤣🤣 huwezi kuwazuia watu kuwa na BBQ. Sijui huyu jamaa anadhani ni akina nani lol.
”Nenda hamia kijijini huko huko usipotaka kusikia harufu ya nyama kwa majirani.”
‘Haki katika ubora wake lol,” mtumiaji mmoja aliandika.”
TAZAMA:WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAGOMA KUFUNGUA MADUKA, HALI ILIVYO, HUDUMA HAKUNA UKIMYA WATAWALA.