Ingawa Guiness haijathibitisha rekodi ya Hilda, mtumiaji wa mtandao wa Twitter aliuliza kwanini Hilda hajatangazwa kama mtu aliyevunja rekodi ya dunia ya Guinness .
Msimamizi rasmi wa ukurasa wao ya Twitter alijibu kwamba wanafahamu jaribio la mwanamke huyo lakini wanakagua ushahidi kabla ya kumtangaza rasmi.
Vitu ambavyo mwanamke huyo anapaswa kuzingatia ili aweze kuvunja rekodi ya dunia ni pamoja na kupika kwa kusimama ambapo haruhusiwi kabisa kukaa wakati anapika.
Pia anaruhusiwa kula chakula, kunywa juisi na maji yaani maji yenye glucose pekee ili kumuongezea nguvu ila haruhusiwi kunywa kahawa au energy drink.
sambamba na hayo akimaliza kupika haruhusiwi kukiuza chakula kwa watazamaji bali anatakiwa kugawa chakula hicho bila malipo.
Mpaka sasa hilda taarifa zake kwenye mitandao mbalimbali ni kuwa amepika kwa masaa zaidi ya 90 na kuandaa vyakula zaidi 115.