Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kuwa watu zaidi ya 670 wameuawa katika mapigano Sudan.
OCHA iimeripoti kuwa watu 670 wameuawa na wengine 5,567 wamejeruhiwa katika mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan, na vikosi vya Radiamali Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Jenerali Muhammad Hamdan Daghalo.
Ripotii zinasema wakazi wa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, wanakabiliwa na ukosefu wa chakula kutokana na wizi, uporaji na kuchomwa moto makumi ya viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Pande zinazozozana huko Sudan tarehe 11 mwezi huu wa Mei zilisaini makubaliano ya kulindwa usalama wa raia na kuruhusiwa operesheni za misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na mapigano.