Chuo cha Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini kimeunga mkono jitihafa zinazofanywa na Baraza la taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi NACTIVET ya kutoamafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo ili kiweza kuwajengea uzoefu wanapopata ajira.
Sekta mbalimbali zinatoa mafunzo kwa vitendo katika maonyesho yanayofanyika Jijini Arusha katika Uwanja Wa Sheikh Amir Abed yenye kaulimbiu isemayo . “Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa nguvu kazi mahiri.
Kumekuwa na ajali nyingi pamoja na majanga ya moto mahala pakazi na majumbani hivyo chuo cha Jeshi la Zimamoto kwa kuliona hilo wamejikita kutia elimu katika jamii ili kupunguza na kuondoa changamoto hizo.
Vilevile wamewaomba wazazi kiwapelka watoto wao katika chuo cha Jeshi la Zimamoto ili waweze kupata elimu na kuisaidia jamii kuondoka na majanga ya moto.
\.