Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan baada ya Yanga SC kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla (aggregate) 4-1 ametangaza ahadi nono.
Rais Samia ametangaza kuwa hatua ya fainali sasa atatoa Tsh milioni 20 kwa kila goli ila timu utoke na ushindi lakini kubwa ametangaza kuwa atatoa ndege kutoka Dar es Salaam hadi Algeria kwenda kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya USM Alger Juni3 2023.
“Nilianza na mechi hizi na milioni 5 kwa kila goli la ushindi, waliposogea nikasema sasa milioni 10 kwa kila goli la ushindi, tunapokwenda fainali ni milioni 20 kila goli timu ikitoka na ushindi sio kafunga moja kafungwa mbili zaidi ya hapo serikali itatoa ndege kuwapeleka katika mchezo wa fainali itabeba wachezaji pamoja na mashabiki”>>> Rais Samia
Yanga SC itacheza fainali dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mfumo wa nyumbani na ugenini, mchezo wa kwanza Yanga ataanzia Dar es Salaam Mei 28 na marudiano ni Juni 3 2023, hatua hii ni kubwa zaidi kwa timu ya Tanzania kuwahi kufika katika michuano hii.